Skip to content

World Food Safety Week – Lawrence Omuhaka: Serikali inahakikisha upatikanaji chakula salama

REF: Lawrence Omuhaka: Serikali inahakikisha upatikanaji chakula salama

Colorful fruits and vegetables colorfully arranged at a local fruit and vegetable market in Nairobi, Kenya.

Katibu mwandamizi katika wizara ya kilimo  Lawrence Omuhaka amekariri kujitolea kwa serikali kuhakikisha kuwa wakenya wote wanapata chakula salama.

Akiongea wakati wa siku ya kimataifa kuadhimisha usalama wa chakula katika kaunti ya Meru, Omuhaka alisema kuwa mipango ya kuwaelimisha wakulima kuhusu usalama wa chakula hasa katika matumizi ya kemikali katika mashamba inaendelea ili kuhakikisha kuwa mavuno yanayopatikana ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Alisema kuwa mipango ya kutoa mafunzo pia italenga kuhakikisha kuwa chakula kinachozalishwa nchini kinaafikia viwango vya kuuzwa katika mataifa ya nje na viwango vya matumizi ya humu nchini.

Katibu huyo aliongeza kuwa utandawazi na kuwekwa huru kwa masoko kumeibua changamoto nyingi za usalama wa chakula.

Kwa upande wake, gavana wa kaunti ya  Meru  Kiraitu Murungi alitoa wito kwa serikali kutafuta mikakati ya kuhakikisha kuwa chakula kinachouzwa na kutumiwa humu nchini kinaafikia viwango sawa na vile vinavyouzwa katika masoko ya kimataifa.